Kikosi cha Simba kitawasili jijini Dar es salaam saa mbili na nusu asubuhi hii wakitokea Mtwara ambako jana walikabidhiwa ubingwa wa ligi kuu waliotwaa kwa msimu wa tatu mfululizo
Shamra shamra za Ubingwa zilifanyika huko Ruangwa baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Kikosi cha Simba kimelala mkoani Mtwara na asubuhi hii 'kinapaa' kurejea jijini Dar es salaam
Shamrashamra za ubingwa zitaanzia uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na zitahitimishwa Makao Makuu ya klabu ya Simba, Msimbazi
ADVERTISE HERE