Mabingwa wa nchi Simba leo watakabidhiwa ubingwa wao walioutwaa kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Lindi
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa tisa Alasiri ili kutoa nafasi ya shamrashamra hizo ambazo mgeni rasmi atakuwa Rais wa TFF Wallace Karia
Nahodha wa Simba John Bocco amesema hawatapenda kuona sherehe yao inavurugwa kwa kupoteza mchezo huo
Kocha Sven Vandenbroeck huenda akafanya mabadiliko ya kikosi chake, akiupigia hesabu mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumapili
Baada ya 'kusepa' na taji la Ligi Kuu, Simba imepania kuondoka na ubingwa wa FA pia
ADVERTISE HERE