Tuko kamili kuikabili Namungo - Bocco

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Jul 2020
Tuko kamili kuikabili Namungo - Bocco

Nahodha wa Simba John Bocco amesema wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa

Mchezo huo utafuatiwa na hafla ya kukabidhi Simba ubingwa wa ligi kuu ambao wameutwaa kwa misimu mitatu mfululizo

Bocco amesema wanafahamu mchezo huo hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa kikosi cha Namungo kitakachokuwa kikicheza katika uwanja wake wa nyumbani

Hata hivyo, amesema ili kunogesha shamrashamra za ubingwa, wanahitaji kushinda

"Tunaiheshimu Namungo ni timu nzuri na ipo kwenye kiwango bora kwa sasa na tunaenda kucheza kwenye uwanja wao tunajua mechi itakuwa ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda"

"Tutafuata maelekezo ya walimu watakayotupa kuelekea mchezo huu na sisi kama wachezaji tunajua umuhimu wa hii mechi na tutahakikisha tunashinda ili sherehe za ubingwa wetu ziwe nzuri," Bocco aliiambia tovuti ya Simba

Baada ya kujiunga na Simba akitokea klabu ya Azam Fc, Bocco ameweka rekodi ya kushinda ubingwa wa ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo

Wakati anasajiliwa na Simba, mchezaji huyo mkongwe alionekana kama muda wake umeisha

Hata hivyo kwa mambo aliyofanya ndani ya kikosi cha Simba katika misimu yake mitatu, heshima yake imeendelea kubaki juu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’