Wakati wakiingia uwanjani kuelekea mchezo dhidi ya Ndanda Fc, wachezaji wa Simba walipewa heshima na wenyeji wao, Ndanda Fc baada ya kutwaa ubingwa mapema kabla ya msimu kumalizika
Nyota wa Ndanda walipanga mstari huku wakiwapigia makofi wachezaji wa Simba pamoja na viongozi wao wa benchi la ufundi ukiwa ni utaratibu unaofanyika kote dunia kwa timu inayoshinda ubingwa mapema
Msimu uliopita Simba ilipata heshima kama hiyo pia baada ya kutwaa ubingwa ikiwa na michezo mitatu mkononi
ADVERTISE HERE