Leo uongozi wa klabu ya Simba utatoa tathmini ya majeraha aliyopata beki mahiri Shomari Kapombe ambaye alifanyiwa vipimo jana
Kapombe aliumizwa na kiungo Frank Domayo kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Azam Fc
Daktari wa Simba Dk Yassin Gembe amesema baada ya nyota huyo kufanyiwa vipimo, leo wanatarajiwa kupokea taarifa itakayobainisha ukubwa wa majeraha hayo
"Mchezaji alifanyiwa vipimo jana, tunatarajia kupokea majibu ya vipimo hivyo leo hivyo ni vyema mashabiki wetu wakawa watulivu.," amesema Dk Gembe
Wakati taarifa hiyo ikisubiriwa, jana uongozi wa Simba ulisema kuwa hali ya Kapombe inaendelea vizuri
ADVERTISE HERE