Uongozi wa klabu ya Simba umewatoa hofu mashabiki wake kuhusu beki Shomari Kapombe ambaye jana alifanyiwa madhambi na kiungo wa Azam Fc Frank Domayo
Domayo alimfanyia Kapombe madhambi ya makusudi kabisa, hata hivyo baada ya kupewa huduma ya kwanza kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, Kapombe aliweza kusimama na kutembea mwenyewe japo kwa kuchechemea
"Kapombe anaendelea vizuri, taarifa rasmi kuhusu majeraha aliyopata itatolewa na madaktari wa Simba baada ya kumfanyia vipimo," amesema
Tukio alilofanya Domayo limelaaniwa vikali na wadau wa soka nchini wakitaka mchezaji huyo achukuliwe hatua
Kapombe hakuwa tayari kuzungumza na Domayo jana baada ya tukio lile, hata hivyo nahodha huyo wa Azam Fc ameomba radhi na kuahidi kumpigia simu leo
ADVERTISE HERE