Afisa Habari na Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema wanafahamu mchezo dhidi ya Azam Fc hautakuwa mwepesi lakini ana matumaini makubwa kuwa wachezaji watailinda heshima ya Simba na kutinga nusu fainali
Azam Fc inatolea macho michuano hiyo waliyotwaa msimu uliopita na kukata tiketi ya kushirikia michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika
Tayari Simba 'imesepa' na taji la ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao, lakini ushindi kwenye mchezo huo una umuhimu mkubwa
Taji la FA ni moja ya kipaumbele msimu huu, lakini pia ushindi unaweza kuwakutanisha na watani zao Yanga kwenye hatua ya nusu fainali kama nao watashinda mchezo dhidi ya Kagera Sugar
"Tunajua Azam Fc watakuja moto sana kesho, lakini sisi ndio mabingwa, sisi ni wakubwa mara milioni yao, tunawaheshimu ila watatusamehe kwa kesho. Katika mechi za Tanzania hii ndio game unaweza kupata burudani ya soka, niwahakikishie tu tupo tayari kwa mtanange huu na Insha'Allah Bingwa wa taifa hili ang’avu atashinda, " kauli Haji Manara
Jana TFF ilitangaza kubadili muda wa mchezo huo kutoka saa kumi jioni na sasa utapigwa saa moja usiku katika uwanja wa Taifa