Ubingwa wampa mzuka Ajibu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Jun 2020
Ubingwa wampa mzuka Ajibu

Kiungo wa Simba Ibrahim Ajibu ameelezea furaha yake baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu

Ajibu aliondoka Simba mwaka 2017 kujiunga na Yanga ambayo aliitumikia miaka miwili bila ya kutwaa taji lolote huku Simba ikishinda mataji mawili ya ligi kuu

Msimu uliopita akarejea klabu ya Simba kwa heshima na hatimaye ameweza kuwa sehemu ya kikosi kllichotwaa ubingwa wa tatu mfululizo ingawa kwake ni taji la kwanza

"Nimefurahi kwa mafanikio haya tuliyopata msimu huu. Kwangu binafsi nilikuwa na kiu kubwa ya kutwaa ubingwa. Niliondoka kwa heshima na nimerudi kwa heshima mahali nilipokuzwa, nimefanikiwa kutimiza ndoto zangu kwa kutwaa taji la heshima la Ligi Kuu, asanteni mashabiki wa Simba, " alisema Ajibu

Ajibu alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao uliwapa Simba ubingwa wao wa tatu mfululizo licha ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana

Simba sasa imeelekeza nguvu kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa uwanja wa taifa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’