Simba kuweka kambi Morogoro kuelekea kombe la Shirikisho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Jan 2018
Simba kuweka kambi Morogoro kuelekea kombe la Shirikisho
Kikosi cha Simba kinatarajia kwenda tena Morogoro au Zanzibar kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuwavaa wapinzani wao katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, klabu ya Gendarmarie Nationale kutoka Djibouti, imefahamika.

Vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanatarajia kuwakaribisha Gendarmarie katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Februari 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. <

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah "Try Again" amesema uamuzi kamili utafanywa katika kikao cha pamoja na benchi la ufundi baada ya kumaliza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Majimaji itakayofanyika Jumapili.

Salim alisema uongozi wa klabu hiyo unaamini kuwa kambi hiyo watakayokaa itasaidia kuwaweka wachezaji tayari kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo wao wa kwanza wa kimataifa ambao utakuwa ni mtihani wa kwanza wa kimataifa kwa kocha mpya Mfaransa, Pierre Lechantre.

"Jumatatu wachezaji watapumzika lakini tutakuwa na kikao na benchi la ufundi kwa ajili ya kuamua kambi itakuwa wapi, kama ni Zanzibar au Morogoro, ila mazoezi wataanza Jumanne na baadaye ndiyo wataingia kambini," alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa mbali na kuandaa timu yao, vile vile wameunda "kikosi kazi" ambacho kazi yake maalumu kuwapeleleza wapinzani kabla hawajafika nchini na hatimaye kujipanga kuwakabili.

Baada ya wiki mbili, Simba itasafiri kuelekea Djibouti kuwafuata wenyeji wao ambao wanatumia uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 40,000.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’