Muda mchache ujao, saa kumi jioni, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kitashuka kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kuikabili Tanzania Prisona katika mchezo ambao matokeo yoyote ya sare au ushindi yataihakikishia Simba ubingwa wa tatu mfululizo
Kama machampioni hao wa Tanzania watapata matokeo chanya, siku ya leo itaingia kwenye historia ya klabu kwa kufanikiwa kuandikisha ubingwa wa 21
Huu ni mchezo muhimu na wa heshima kwa Simba, ndio maana hata mamlaka za Serikali zimeruhusu mashabiki kuingia kuushuhudia
Bila shaka wachezaji watawapa furaha mashabiki na watatimiza kiu yao ya kuona wanachukua ubingwa mapema na kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa wakiwa na mechi sita mkononi
Kila la kheri Simba, kila la kheri mabingwa wa nchi...
ADVERTISE HERE