Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba jioni ya leo wanashuka kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kumenyana Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Katika mchezo huo Simba inahitaji angalau alama moja tu kuwa rasmi mabingwa kwa msimu wa tatu mfululizo
Ingawa kimahesabu, Simba ni kama ilitwaa ubingwa huo tangu jana kwani utajiri wao wa mabao waliyofunga, utawabeba hata ukitokea 'muujiza' wa kupoteza mechi zote saba zilizobaki
Habari njema kwa mashabiki wa Simba mkoani Mbeya , ni kuwa wataruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo huo ingawa ni kwa idadi maalum
Mapame wiki hii Serikali ilitangaza kuzuia mashabiki kuingia uwanjani katika mechi za Simba na Yanga kutokana na ugumu wa kuwadhibiti wakati huu wa changamoto ya corona
cutKocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake wako tayari kuwapa burudani mashabiki wao lakini kubwa zaidi ni kuondoka na kombe mkoani Mbeya
"Nina uhakika kesho (leo) tutacheza mchezo mzuri. Kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo na hilo ni jambo zuri kwa kocha kuchagua mchezaji yeyote. Tutacheza kushinda na kama matokeo yakiwa chanya tutapata kitu cha ziada na hilo ndio lengo letu," alisema