Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck leo anatarajiwa kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Sokoine
Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa Simba kwani matokeo ya ushindi yatawahakikishia miamba hao wa soka nchini kutwaa taji la ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo na hivyo 'kusepa' nalo moja kwa moja
Sven amesema hatabadili chochote katika maandalizi yake ya mwisho, zaidi atawaongezea mbinu wachezaji wake pamoja na kuwapa muda wa kutosha wa kupumzika
"Hatutabadili chochote, kwetu huu ni mchezo wa kawaida kama ilivyo mingine. Jana tulifanya mazoezi magumu kwa wachezaji ambao hawakucheza juzi na wengine wakifanya mazoezi ya recovery baada ya mchezo. Leo tutakuwa na muda wa kujiandaa kimbinu zaidi, tutapitia mikanda ya video ya wapinzani wetu," alisema Sven
Mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo ambao ulipigwa jijini Dar es salaam, ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana