Kiu yetu ni kutwaa ubingwa - Miraji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Jun 2020
Kiu yetu ni kutwaa ubingwa - Miraji

Kikosi cha Simba leo kimejifua katika uwanja wa Sokoine yakiwa ni maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi

Mshambuliaji Miraji Athumani alikuwa miongoni mwa nyota waliojumuika katika mazoezi hayo yaliyoanza mapema asubuhi

Akizungumza baada ya mazoezi, Miraji alisema ari ya wachezaji iko juu wakiwa na shauku kubwa ya kumaliza kazi siku ya Jumamosi

"Tuko vizuri, malengo yetu ni kuhakikisha tunapata ushindi dhidi ya Prisons na kuwa mabingwa. Litakuwa jambo la furaha kwangu kushinda ubingwa nikiwa na klabu ya Simba," alisema

Aidha akizungumzia kukataliwa kwa bao lake alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City, Miraji ameeleza kuwa mpaka sasa hajaelewa kwa nini bao lile lilikataliwa

"Kiukweli niliumia sana baada ya bao lile kukataliwa kwani nilidhani nimejiongezea hesabu katika mabao yangu ya msimu huu. Lakini waamuzi ndio wenye kauli ya mwisho"

Kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu, Miraji aliifungia Simba mabao sita, idadi ambayo imeendelea kubaki hivyo baada ya bao lake kukataliwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17m ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
18h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’