Nahodha wa Simba John Bocco jana ameendeleza kasi yake, akifunga mabao yote katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopiga mkoani Mbeya
Mkongwe huyo sasa amefikisha mabao sita. Bocco 'amenoga' wakati msimu ukielekea ukingoni
Mwanzoni mwa msimu alikosekana karibu miezi minne kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc
Kwa sasa anaonekana kuwa chaguo la kwanza kwenye safu ya ushambuliaji jana akianza na Miraji Athumani ambaye nae aliingia kambani kwenye dakika za majeruhi lakini bao lake likakataliwa na waamuzi
Bocco amesema siri ya mafanikio yake ni juhudi pamoja na ushirikiano anaopata kutoka kwa wachezaji wenzake
"Tuna malengo ya timu, kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu. Hivyo tunapopata matokeo ni jambo jema kwetu. Kwangu jukumu kubwa ni kuisaidia timu, " alisema Bocco baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City
Simba inaweza kuondoka na ubingwa mkoani Mbeya kama itashindwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumamosi