Mlinda lango wa Simba Beno Kakolanya amepewa program maalum ya mazoezi ili kuboresha kiwango chake kabla ya kurejeshwa kikosini
Baada ya ligi kurejea kutoka kwenye mapumziko ya corona, nyota huyo aliyesajiliwa kutoka klabu ya Yanga, alionekana kutokuwa 'fit'
Inaelezwa Kocha Sven Vandenbroeck alimpa program maalum ya mazoezi kama alivyofanya kwa wachezaji wengine
Aidha wakati kipa namba moja Aishi Manula akiendelea kufanya vizuri, chipukizi Ally Salim naye alirejea akiwa na 'moto mkali' na hivyo kumpiku Kakolanya kwenye nafasi ya kipa namba mbili
ADVERTISE HERE