Djuma afurahia 'maujuzi' ya Mfaransa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
25 Jan 2018
Djuma afurahia 'maujuzi' ya Mfaransa
Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema kikosi chao kipo fiti kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao watacheza Jumapili dhidi ya Majimaji, Uwanja wa taifa jijini hapa.

Simba ipo kwenye maandalizi ya kuelekea mchezo huo wa kumalizia mzunguko wa kwanza chini ya kocha wao mkuu, Pierre Lechantre ambaye alianza rasmi kukinoa kikosi hicho jana Jumatano.

Kikosi hicho cha Mfaransa, Pierre Lechantre chenye pointi 32 kileleni mwa msimamo, kitacheza mchezo huo kikiwa na faida ya mahasimu wao, Yanga kutangulia kucheza Jumamosi dhidi ya Azam.

“Tunaenda kukutana na timu yenye kocha ambaye alinifundisha, mchezo huo tunauchukulia kwa uzito sana kwa sababu hakuna sehemu nyingine ambayo tunatizama zaidi ya ligi kwa upande wa mashindano ya ndani.

“Mategemeo yetu ni kupata matokeo ya ushindi ili tumalize mzunguko wa kwanza kwenye nafasi ya juu,” alisema kocha huyo msaidizi wa Simba.

Hata hivyo Masoud ameuzungumzia ujio wa kocha mkuu kwenye kikosi cha Simba kwa kusema ameufuraia na ameweka wazi kuwa atampa ushirikiano wa kutosha.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
10h ago
READ MORE →
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
10h ago
READ MORE →
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
13h ago
READ MORE →
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE →
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE →