Kiungo fundi Jonas Mkude amewatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa anaendelea vizuri na huenda akarejea dimbani mapema
Baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC, ilitangazwa Mkude angekaa nje kwa wiki mbili akiuguza majeraha hayo
Hata hivyo ameshaanza mazoezi mepesi huku akibainisha kuwa hali yake inaendelea vizuri
"Maendeleo yangu ni mazuri, kwa sasa nafasnya taratibu za kimatibabu nikisimamiwa na wataalam ili niweze kupona kabisa ili niendelee na majukumu yangu," alisema
Mkude atakosa mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons lakini huenda akarejea kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Julai Mosi 2020
ADVERTISE HERE