Kikosi cha Simba kimewasili mkoani Mbeya tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa keshokutwa Jumatano katika uwanja wa Sokoine
Mabingwa hao wanaosubiri kutangazwa, waliondoka jijini Dar es salaam mapema leo kwa usafiri wa ndege
Wanakabiliwa na mechi mbili mkoani Mbeya, mechi ambazo kama watashinda zote wanaweza kutangaza ubingwa mapema tu kwani mpaka sasa wanahitaji alama nane kutoka mechi nane zilizobaki

ADVERTISE HERE