Inaelezwa mabosi wa klabu ya Simba wamewapiku watani zao Yanga baada ya kumnasa aliyekuwa mshambuliaji wa Rayon Sport Michael Sarpong raia wa Ghana
Sarpong yuko huru baada ya kuvunja mkataba wake na Rayon kuvunjwa baada ya kutokea sintofahamu baina yake na viongozi wa klabu hiyo
Habari za kuaminika kutoka chanzo makini ndani ya uongozi wa Simba, zimefichua kuwa Sarpong atasaini mkataba wa miaka miwili
Nyota huyo atawasili nchini wakati wowote ili kukamilisha dili hilo
Akiwa Rayon, Sarpong aliifungia timu hiyo mabao 24 katika misimu miwili aliyocheza. Mpaka mkataba wake unavunjwa, alikuwa amefunga mabao nane
Simba imepania kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
ADVERTISE HERE