Kiungo fundi Ibrahim Ajib asubuhi ya leo alifunga mabao mawili katika mchezo wa kirafiki ambao Simba ilicheza dhidi ya African Lyon katika dimba la Uhuru na kuibuka na ushindi wa mabao 5-0
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amejiwekea utaratibu wa kuwapa wachezaji wote muda wa kucheza kwa kuweka mechi za kirafiki kila baada ya mchezo wa kimashindano
Mechi hizo huwashirikisha zaidi wachezaji ambao hawakupata nafasi katika mchezo uliopita pamoja na wale waliocheza kwa muda mchache
Sven amesema anahitaji wachezaji wake kucheza angalau dakika 70 kila mechi ili kuwarejesha katika ushindano waliokuwa nao kabla ya janga la corona
Mabao mengine yalifungwa na Tairone Da Silva, Mzamiru Yassin na Deo Kanda
ADVERTISE HERE