Sven awataka kina Ndemla 'wasipoe'

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Jun 2020
Sven awataka kina Ndemla 'wasipoe'

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema anafahamu mashabiki wanapenda kuwaona wachezaji wanaowapenda wakipata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza mara kwa mara

Hata hivyo amesema kila mchezaji anapaswa kupambana ili kustahili kupewa nafasi ya kuonekana kikosini

Jana Sven aliwapa nafasi kiungo Said Khamis Ndemla na Yusufu Mlipili katika mchezo dhidi ya Mwadui Fc na mabingwa hao watetezi kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-0

Ndemla aling'ara sana kwenye mchezo huo akishirikiana vyema na Gerson Fraga katika eneo la kiungo

Sven amewataka wachezaji hao wapambane zaidi ili aendelee kuwapa nafasi kwenye kikosi cha kwanza

"Nafahamu watu wanafurahi kumuona Ndemla na Mlipili, kwenye mahojiano mengi naulizwa maswali yanayojirudia kuhusu majina hayo na mengine"

"Niliwaambia wachezaji wangu wakati tunaanza mazoezi baada ya mapumziko ya Corona, kama utajituma na kunionesha uwezo mazoezini utapata nafasi"

"Kila mmoja anapaswa kufanya kazi kwa asilimia zote sio 60% wala 70% kwa sababu mwisho wa ligi ndio bingwa anakabidhiwa kombe kwa hiyo wakati huu bado tunahitaji kuwa makini," alisema

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
17h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’