Kagere awatoa hofu wanaohoji kasi yake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Jun 2020
Kagere awatoa hofu wanaohoji kasi yake

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere amesema amejiwekea malengo ya kuvunja rekodi yake ya mabao 23 aliyoweka msimu uliopita

Pamoja na kutokuweka bao kambani kwenye mchezo uliopita, Kagere amesema hilo halimsumbui kwani anaamini atapata nafasi nyingine katika mechi zijazo

"Kama mshambuliaji, nimejiwekea malengo ya kufanya zaidi, hivyo hata ikitokea sijafunga katika mechi tano mfululizo hilo halinisumbui kwani najua wakati wangu utafika," amesema

"Jukumu langu la kwanza ni kuhakikisha timu inapata matokeo bila ya kujali nimefunga au la. Huwa napambana zaidi nifunge lakini hata nisipofunga, basi nitoe usaidizi kwa wenzangu waweze kufunga"

Kagere amepachika mabao 19 mpaka sasa, anahitaji kufunga mabao manne tu kuweza kuifikia rekodi yake ya msimu uliopita ingawa Wanamsimbazi wanatamani kuona anafunga angalau mabao nane ili kuweza kuweka rekodi mpya ya mabao ya muda wote

Kesho Jumamosi, Kagere atakiongoza kikosi cha Simba kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa uwanja wa Taifa kuanzia saa kumi kamili jioni

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
39m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’