Kiungo fundi wa Simba, Msudan Sharaff Elden Shiboub bado ameshindwa kurejea nchini, suala la kufungwa mipaka ya Sudan likiwa changamoto
Hivi karibuni Msemaji wa Simba Haji Manara alisema wanafanya utaratibu mwingine wa kumuwezesha nyota huyo kurejea haraka
Huenda Shiboub atakosa mechi zilizobaki huku pia ikiwa hatma yake ndani ya kikosi cha Simba haifahamika
Mkataba wake na mabingwa hao wa nchi unamalizika katika kipindi cha wiki mbili zijazo ingawa mazungumzo ya mkataba mpya yalishaanza kabla ya janga la corona
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji aliwahakikishia Wanamsimbazi kuwa hakuna mchezaji ambaye ataondoka Simba na klabu hiyo itamsajili mchezaji yeyote ambaye atapendekezwa na kocha Sven Vandenbroeck
ADVERTISE HERE