Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kinafanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema leo Alasiri watafanya mazoezi ya mwisho tayari kwa mchezo huo
"Vijana wote wako katika hali nzuri. Alasiri ya leo tutafanya mazoezi ya mwisho kujiweka tayari kwa mchezo. Huu ni mchezo muhimu sana kwetu, tunahitaji ushindi. Tulipoteza mchezo wa kwanza kule Shinyanga hivyo hii ni nafasi yetu kupata matokeo nyumbani," amesema
Kwenye mchezo wa kesho, Simba itaendelea kumkosa kiungo Jonas Mkude ambaye anaendelea na program maalum ili kupona majeraha aliyopata wiki iliyopita
ADVERTISE HERE