Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema kikosi cha Simba kitaendeleza makali yake kuelekea mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Majimaji utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapil, Januari 28.
Djuma amesema mbali na kusaka ushindi kwenye mechi za Ligi Kuu, pia wanaiandaa timu hiyo na mechi za mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika zitakazofanyika kuanzia mapema mwezi ujao.
Djuma amesisitiza kuwa kila mchezaji anafahamu ushindani ambao uko kwenye ligi, hivyo kila mchezo wanaoshuka uwanjani kucheza, wanatakiwa kupambana kusaka ushindi na si jambo lingine.
"Tumeshinda mechi zilizopita, sasa akili yetu ni kushinda pia na mechi zinazofuata, tunajua kila timu inapambana ili mwisho wa msimu ibebe kikombe, sisi pia hilo ndio lengo letu," alisema kocha huyo.
Aliongeza kuwa uamuzi wa kuimarisha benchi la ufundi kwa kumleta Kocha Mkuu Mfaransa, Pierre Lechantre, ni kutaka kuhakikisha Simba inachukua ubingwa wa ligi na kufika mbali katika michuano ya Afrika na ikiwezekana kunyakua taji hilo kwa mara ya kwanza.
"Wachezaji wanajua na kila siku tunawaeleza kwenye mazoezi kwamba hakuna timu ndogo kwenye ligi au mashindano yoyote, wanatakiwa kupambana kusaka ushindi kama vile hakuna mechi nyingine, leo sisi tunaongoza ligi, wenzetu pia wanaitaka hiyo nafasi, kikubwa ni kushinda mechi zinazofuata na hakuna atakayetukamata," aliongeza kocha huyo.
Simba ina rekodi ya kutofungwa msimu huu wa 2017/18 tangu ulipoanza Agosti mwaka jana ndio vinara wa ligi hiyo yenye timu 16 wakati Majimaji wenye pointi 12 wako katika nafasi ya 13 katika msimamo.
Mechi mbili za mwisho Simba imepata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Singida United na mabao 2-0 ilipokuwa ugenini kuifuata Kagera Sugar wakati Majimaji imetoka sare ya bao 1-1 mara mbili ilipowakaribisha Azam FC na Singida United.

ADVERTISE HERE