Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesisitiza kuwa klabu hiyo haikuwahi kufanya mazungumzo na winga wa Yanga Bernard Morrison
Manara amesema Simba haijaanza michakato ya usajili, kwa sasa wameweka mkazo katika kutetea ubingwa
"Sisi hatujaanza usajili, hiyo taarifa ya kuwa tumempa pesa Morrison mmeitoa wapi?," alihoji Manara wakati akizungumza na Wasafi FM
"Simba hatuna cheo cha Rais wala hatuna Wakala, hivyo jambo hilo ni uzushi mtupu"
"Kwa sasa mkakati wetu ni kuhakikisha tunamaliza mechi zilizobaki salama ili kutetea ubingwa kisha ndio tuanze usajili. Hatukuwahi kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, kwa kuwa huu sio wakati wake. Na tutakapoanza usajili wachezaji tutakaowasajili ni wale waliopendekezwa na kocha"
"Kama atamtaka Morrison na akiwa hana mkataba na klabu yoyote tutamsajili, fedha tunayo," alitamba Manara
"Taarifa hizo mnatoa ili kujifurahisha tu lakini mnafahamu hazina ukweli wowote. Acheni kuzusha taarifa zenye lengo la kuichafua Simba, mfahamu klabu hii ndio bingwa wa nchi yenu na mabingwa wa kihistoria ukanda huu wa Afrika Mashariki"