Sven ataka umoja Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Jun 2020
Sven ataka umoja Simba

Pamoja na sare ya bao 1-1 katika mchezo wa juzi dhidi ya Ruvu Shooting, Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck, amewataka mashabiki wa timu hiyo waendelee kuiunga mkono timu yao ili waweze kutimiza malengo

Jana Simba ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp na kupata ushindi wa mabao 4-0, mchezo ambao ulipigwa uwanja wa Uhuru

Katika mchezo huo Sven alitumia wachezaji ambao hawakucheza juzi na wale ambao walicheza dakika chache

Baada ya mchezo, Sven alisema pamoja na timu yake kushinda mchezo huo, bado wanahitaji kuongeza stamina na 'fitnes' ya wachezaji ili kuweza kurejesha kiwango walichokuwa nacho kabla ya ligi kusimama

"Tumeshinda mechi zote za kirafiki lakini bado tunahitaji kujiimarisha. Juzi hatukuweza kushinda mchezo wa ligi lakini nadhani hatupaswi kulaumiana kwa kuwa ni kawaida kwenye mchezo wa soka, tunapaswa kuwekeza nguvu kwenye mchezo ujao"

"Wachezaji walipambana kupata ushindi lakini matokeo hayakuwa mazuri sana. Hakuna haja ya kumlaumu mchezaji yoyote, mashabiki lazima waelewe matokeo kama haya yanatokea kwenye mpira, nimewataka wachezaji wangu sasa kuelekeza mawazo yao kwenye mchezo ujao," alisema Sven

Simba itashuka kwenye uwanja wa Taifa siku ya Jumamosi kuumana na Mwadui Fc kwenye mchezo wa mzunguuko wa 30

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’