Waziri Mkuu 'aifagilia' Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Jun 2020
Waziri Mkuu 'aifagilia' Simba

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mh Kassim Majaliwa ameipongeza klabu ya Simba kwa mafanikio iliyopata katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni

Jana wakati akiwasilisha hotuba yake ya kuhitimisha bunge la Bajeti, Mh Majaliwa alisema mafanikio iliyopata Simba na hata sasa ikikaribia kutwaa ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo, ni wazi haina mshindani hapa Tanzania

"Simba inakaribia kutangaza ubingwa ikiwa na michezo mingi mkononi, sasa nini faida ya mkuki?, " alisema Waziri Mkuu ambaye alikuwa akijibu tambo za Waziri wa Fedha Mh Philip Mpango alizotoa juzi Bungeni hapo akizungumzia ushindi waliopata Yanga dhidi ya Simba

"Mfungaji anayeongoza kwenye ligi ni Meddie Kagere aliyefunga mabao 19, hatujaona timu ya Wananchi ikiongoza kwenye mabao"

"Msimu mmoja nyuma, Simba iliandika historia kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kwa kufanikiwa kutinga hatua ngumu ya robo fainali, haya ni mafanikio ambayo hakuna timu imeyapata katika kipindi cha miaka 15"

Kauli hiyo ya Waziri Mkuu iliamsha shangwe kutoka kwa wabunge pamoja na Spika wa Bunge Mh Job Ndugai ambaye ni Mwanachama wa klabu ya Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’