Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting jana, kikosi cha Simba leo kiliendelea na mazoezi ambapo baadhi ya wachezaji ambao hawakupata nafasi jana na wale waliocheza kwa muda mfupi, walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Uhuru, uliishuhudia Simba ikiondoka na ushindi wa mabao 4-0
Mabao ya Simba yaliwekwa kambani na Ibrahim Ajib, Gerson Fraga aliyefunga mabao mawili na Cyprian John
Simba inaendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Juni 20 kwenye uwanja wa Taifa








ADVERTISE HERE