Winga wa Simba, Shiza Kichuya, amedhihirisha kuwa bado wamo baada ya jana kufunga bao maridadi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1
Kabla ya kufunga bao hilo, Kichuya alipiga shuti lililotemwa na kipa Mohammed Makaka na mpira kumrudia na kuutumbukiza nyavuni
Kiwango alichoonyesha kilikuwa bora kulinganisha na mechi za mwanzo wakati aliporejea Simba akitokea nchini Misri
Kichuya aliahidi kuwa ligi itakaporejea Wanasimba watamuona katika uhalisia wake kama walivyomzoea
Nyota huyo amefichua kuwa alilazimika kufanya mazoezi ya kupunguza uzito pamoja na kufanya mazoezi maalum ambayo yamemuongezea stamina na taratibu kuanza kurejesha kasi yake
Jana kocha Sven Vandenbroeck alimuanzisha wingi ya kushoto na baadae kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Francis Kahata