Mshambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere, kinara wa mabao VPL, leo atakuwa na nafasi ya kuendelea kuifukuzia rekodi ya mabao ya miaka mingi iliyowekwa na Mohammed Hussein
Katika mechi 10 zilizobaki, Kagere atahitaji kufunga mabao nane ili kuweka rekodi yake ya mabao ya muda wote ligi kuu ya Tanzania Bara
Mwamba huyo raia wa Rwanda aliyekulia nchini Uganda, yuko fiti na huenda leo atafanya kile kinachosubiriwa na wengi
Mabao yake 19 aliyofunga mpaka sasa, yanampa kila sababu ya kuvunja rekodi hiyo ya mabao 26 kwenye mechi 10 zilizobaki
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema anaamini Kagere ataweza kuivunja rekodi hiyo kama ataendeleza kasi yake aliyokuwa nayo kabla ya ligi kusimama kutokana na corona
Katika mchezo dhidi ya Singida United ambao Simba ilishinda kwa mabao 8-0, Kagere aliingia kambani mara nne na kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika mechi moja msimu huu