Mabingwa wa nchi Simba jioni ya leo Jumapili watakuwa uwanja wa Taifa kuwapa burudani mashabiki wao watakapowakaribisha Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kukosa burudani kwa takribani miezi mitatu, mashabiki leo watakuwa na nafasi ya kuwashuhudia mabingwa hao watarajiwa wakifanya yao
Ni mchezo ambao Simba inahitaji kushinda katika mkakati wake wa kutangaza ubingwa baada ya mechi tano
Simba itaingia uwanjani leo ikiwa na kikosi chake kamili kilichoiva baada ya kujifua pamoja kwa wiki mbili
Viungo Jonas Mkude (majeruhi) na Sharaf Shiboub (hajarudi) ndio wachezaji pekee ambao hawako kwenye mpango wa mwalimu kwa ajili ya mchezo huo
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao kuhakikisha ushindi unapatikana
Amesisitiza kila shabiki anapaswa kuzingatia tahadhari ya corona kwa kuvaa barakoa pamoja na kunawa mikono
Utaratibu wa ukaaji majukwaani pia utazingatia umbali wa mita moja kati ya shabiki na shabiki