Wataka kocha mpya asivuruge mfumo wa Djuma

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Jan 2018
Wataka kocha mpya asivuruge mfumo wa Djuma
Kocha mpya wa Simba Pierre Lechantre leo ameanza rasmi kukinoa kikosi cha Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuchukua mikoba ya Joseph Omog aliyetimuliwa hivi karibuni.

Baada ya kutimuliwa Omog wakati ikifanya mchakato wa kupata kocha mpya, Simba ilikabidhiwa mikononi mwa kocha msaidizi Masudi Djuma.

Kocha huyo raia wa Burundi alifanya marekebisho makubwa ya mfumo wa uchezaji kwa kikosi chake kutoka ule 4-4-2 au 4-3-3 wa Omog na kutumia 3-5-2.

Awali mfumo huo ulionekana kuwasumbua wachezaji hadi kupelekea kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi.

Hata hivyo sasa wachezaji wanaonekana kufahamui filisofia ya mfumo huo kwani matunda yake yameanza kuonekana kwenye ligi.

Djuma ameiongoza Simba kwenye michezo mitatu ya ligi na Simba imeshinda michezo yote bila ya kuruhusu hata bao moja.

Ilianza kuilaza Ndanda Fc mabao 2-0, ikaja ikaichapa Singida United 4-0 na juzi kuilaza Kagera Sugar mabao 2-0 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mjadala uliozuka miongoni mwa mashabiki wa Simba ni hofu ya kuvurugika kwa mwendelezo wa ushindi uliowekwa na Djuma baada ya kuanza kutumia mfumo wa 3-5-2 ambao sasa unaeleweka vizuri na wachezaji.

Lechatre hana kawaida ya kutumia mfumo wa wachezaji watatu nyuma na haifahamiki kama atakuwa tayari kutumia mfumo ambao mwenyewe haupendelei.

Wapo waliokwenda mbali na kushauri ingekuwa vyema kama Djuma angeachwa aiongoze Simba mpaka mwishoni mwa msimu halafu Lechantre akakabidhiwa timu mwezi Juni.

Hata hivyo kwa CV ya Lechantre hakuna haja ya kuwa na hofu yoyote.

Tayari ameelezea kuvutiwa na uchezaji wa Simba hivyo anaweza kuendeleza alipoishia Djuma. Amesema Simba inakosa kasi tu na hiyo ndiyo kazi yake ya kwanza kuhakikisha anaongeza kasi katika kushambulia.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
7h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
7h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
10h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’