Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewataka mashabiki wa soka nchini kuzingatia kanuni za afya zilizowekwa ili kufurahia ligi kwa usalama
Mashabiki wametakiwa kuingia uwanjani mapema wakiwa wamevaa barakoa ili kuepuka misongamano
Aidha katika viwanja vyote, kutakuwa na sehemu za kunawa/vitakasa mikono ambapo kila shabiki anapaswa kunawa mikono yake
Ndani ya uwanja, mashabiki wametakiwa kukaa umbali wa mita moja kati yao na pia wahakikishe, wanaposhangilia hawagusani
Mikiki mikiki ya ligi kuu inaanza rasmi leo kwa mechi mbili kupigwa
Mwadui Fc inacheza na Yanga mkoani Shinyanga wakati Coastal Union watakuwa wenyeji wa Namungo Fc mkoani Tanga
Mabingwa watetezi Simba wao watashuka dimba la Taifa kesho Jumapili kuwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting