Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa dirisha la usajili kuelekea msimu wa 2020-21, litafunguliwa August 01 mpaka August 31
Katika taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, imebainisha kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya mabadiliko ya tarehe ya kumaliza msimu kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona
Msimu wa VPL 2019-20 utahitimishwa Julai 31 2020
Aidha TFF imewaagiza wachezaji ambao watamaliza mikataba katika vilabu vyao kabla ya Julai 31, wanapaswa kuendelea kuzitumika timu zao mpaka pale msimu utakapofika mwisho
Maelekezo hayo yametolewa na FIFA
ADVERTISE HERE