Mabingwa wa nchi Simba wameendelea kujifua katika uwanja wao wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa siku ya Jumapili, uwanja wa Taifa
Ni mchezo ambao Simba inahitaji ushindi ili kuukaribia zaidi ubingwa wa tatu mfululizo
Kocha Mkuu wa vinara hao wa ligi, Sven Vandenbroeck ameendelea na mkakati wake kuhakikisha timu yake inaweza kushinda mechi zote tano za kwanza ili kutangaza ubingwa mapema na kujikita kwenye michuano ya kombe la FA
Alama 14 zitatosha kuipa Simba ubingwa wa tatu
ADVERTISE HERE