Bocco afunguka hesabu kali za Simba kuelekea mchezo wa Ruvu Shooting

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Jun 2020
Bocco afunguka hesabu kali za Simba kuelekea mchezo wa Ruvu Shooting

Nahodha wa Simba John Bocco, amesema kwa sasa hawafikiri jambo lolote zaidi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Jumapili hii, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bocco amesema baada ya kukaa kwa zaidi ya miezi miwili bila ya kucheza mpira, wanafahamu mwendelezo wa ligi hiyo utakuwa ni mgumu kwa sababu kuna timu zinapambana ili zisishuke daraja.

Bocco alisema timu zinazopigania kubaki kwenye ligi msimu ujao zimefanya maandalizi mazuri ili kuhakikisha zinashinda michezo yao, kuliko zile zinazowania ubingwa.

"Ligi  lazima itakuwa ngumu tu, tena tunaweza kukutana na mambo ambayo hatukuwahi kukutana nayo kwenye mechi 28 tulizocheza,   kutokana na hili akili zetu zote tumeelekeza katika mechi yetu dhidi ya Ruvu ambayo ndiyo ipo karibu, "alisema Bocco.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 23, mwaka jana, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,  Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Kwa sasa Simba  wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 71, huku Ruvu Shooting ikishika nafasi ya 11 kwa pointi 39, baada ya kucheza michezo 28

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’