Msemaji na Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema utafika wakati ataondoka Simba hivyo tayari ameanza kumuandaa mtu ambaye atachukua nafasi yake
"Atakuja msemaji mahiri kuzidi mimi, Sasa tunamuandaa lakini nawaambia huyo mtu ni hatari zaidi yangu"
"Mimi nakwenda kufanya mambo makubwa ya kitaifa lakini sio mwaka huu bado nipo Sana," aliongeza Manara
Manara amekuwa chachu ya umaarufu wa Simba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
Mchango wake katika uhamasishaji ulionekana zaidi mwaka juzi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, ambayo Simba ilifika hatua ya robo fainali
ADVERTISE HERE