Kiungo fundi wa Simba Jonas Mkude huenda akarejea kikosi mapema kuliko ilivyokuwa ikidhaniwa kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC ambao ulipigwa mapema wiki hii katika uwanja wa Mo Simba Arena
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema nyota huyo alipata majeraha ya kawaida na pengine ndani ya wiki hii anaweza kuendelea na mazoezi
"Mkude hajaumia sana hajavunjika wala kupasuka mfupa alipata uvimbe kidogo na yupo kambini na siku mbili zijazo ataanza mazoezi," amesema Manara
Pamoja na kuwa huenda akaukosa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Simba ina uhakika wa kupata huduma ya kiungo huyo mkabaji bora zaidi nchini katika mechi zitakazofuata
ADVERTISE HERE