Pamoja na kushinda michezo miwili waliyocheza katika siku moja, kiungo wa Simba Francis Kahata amesema bado hawajafikia katika ubora wao
Juzi Simba ilicheza mechi mbili ndani ya masaa 10. Asubuhi ikicheza na Transit Camp na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 na jioni yake ikaichakaza KMC mabao 3-1
Kahata amesema pamoja na viwango vya wachezaji kuimarika, lakini bado hawajafika pale ambapo waliishia kabla ya janga la corona
"Ni kweli juzi tumecheza asubuhi na jioni na zote tumeibuka na ushindi, lakini ninachoona ni kwamba wachezaji bado hatujafikia kwenye ule ubora ambao tuliishia nao kabla ya janga hili, lakini taratibu tunaanza kurejea," amesema
Kahata amesema anaamini watakuwa bora zaidi siku ya Jumapili, ligi itakaporejea wakiumana na Ruvu Shooting