Matola ataja siri ya mechi mbili ndani ya masaa 10

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Jun 2020
Matola ataja siri ya mechi mbili ndani ya masaa 10

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema juzi waliamua kucheza mechi mbili za kirafiki katika siku moja ili kupima utimamu wa wachezaji baada ya mazoezi ya takribani siku 10

Juzi asubuhi Simba ilicheza dhidi ya Transit Camp na kushinda mabao 4-2 na jion yake ikacheza na KMC pia ikaibuka na ushindi wa mabao 3-1

Matola amesema mechi hizo waliziandaa siku moja kwa lengo hilo la kuangalia utimamu wa wachezaji kabla ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa Uwanja wa Taifa, Jumapili ijayo

"Tuna kikosi kipana ndio maana tuliandaa michezo ile ndani ya masaa kumi ili kuangalia ni kwa kiasi gani kila mchezaji ameimarika baada ya kufanya mazoezi kwa wiki nzima," alisema Matola

"Mchezo dhidi ya KMC ulikuwa mzuri zaidi kwetu kwani walitupa ushindani mkubwa lakini mwisho wa siku tuliweza kuibuka na ushindi"

Matola amesema kikosi chao kiko tayari akiwataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa siku ya Jumapili kushuhudia burudani kutoka kwa timu yao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
42m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’