Beki KMC amuomba radhi Mkude

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Jun 2020
Beki KMC amuomba radhi Mkude

Beki wa KMC Kelvin Kijili amemuomba radhi kiungo wa Simba Jonas Mkude baada ya kumfanyia madhambi yaliyopelekea nyota huyo kukimbizwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu

Kijili amesema halikuwa kusudio lake kumuumiza Mkude katika mchezo wa kirafiki ambao ulipigwa juzi kwenye uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju jijini Dar es salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1

"Namuomba radhi Mkude kwani halikuwa lengo langu kumuumiza. Ilikuwa katika jitihada za kuwania mpira kwa bahati mbaya yeye alipiga chini ya kiatu changu na kuumiia vidole. Nitamtafuta, nimuombe radhi na namtakia kila la kheri aweze kupona haraka ili aendelee na majukumu yake. Mpira ndio kazi yetu na nafahamu kuna maisha nje ya mpira," alisema Kijili

Mkude alipatiwa matibabu ya awali Hospitali ya Rabininsia Memorial kisha kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako ndiko anatibiwa sasa

Fundi huyo wa mpira amesema ameumia vidole vya mguu wa kulia na amekuwa na maumivu makali tangu juzi

Daktari wa Simba Dk Yassin Gembe amesema bado hawajabaini ukubwa wa jeraha la kiungo huyo, atafanyiwa vipimo baada ya saa 72

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’