Haikuwa rahisi kufunga mabao 19 - Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jun 2020
Haikuwa rahisi kufunga mabao 19 - Kagere

Mshambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere amesema halikuwa jambo jepesi kwake kufunga mabao 19 msimu huu mpaka sasa

Kagere ambaye msimu uliopita aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 23, anaelekea kushinda kiatu cha dhahabu kwa msimu wa pili mfululizo akiwa amefunga mabao nane zaidi ya wachezaji wanaomfuata

"Msimu huu haukuwa rahisi kwangu. Kuna wakati nilikuwa nashindwa kufunga kwa sababu mabeki wananikamia sana. Kila wanaponiona kikosini, huwa wanakamia kuhakikisha sifungi"

"Wengine huwa wanapeana majukumu kwa ajili ya kunifuatilia kila nilipo uwanjani. Naifurahia hali hiyo kwani ikitokea napata nafasi sifanyi makosa," amesema Kagere

Kagere aliyetua Simba misimu miwili iliyopita akitokea klabu ya Gor Mahia ya Kenya, anapigiwa chapuo kuvunja rekodi ya mida wote ligi kuu ya Tanzania Bara

Rekodi hiyo ya mabao 26, inashikiliwa na Mohammed Hussein mkongwe aliyewahi kutamba miaka ya tisini akicheza timu za Yanga na Majimaji

Kagere anahitaji kufunga mabao saba tu kutoka mechi 10 zilizosalia kuweza kuifikia rekodi hiyo

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’