Dk Gembe afunguka majeraha ya Mkude

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jun 2020
Dk Gembe afunguka majeraha ya Mkude

Jana katika mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya KMC, kiungo fundi wa Simba Jonas Mkude alipata majeraha ambayo yalimlazimu kukimbizwa Hospitali ya Rabininsia Memorial

Kwenye mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 ikiwa ni mchezo wa pili kwa siku ya jana ambapo asubuhi Simba ilicheza mchezo mwingine na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2

Habari njema ni kuwa Mkude tayari ameruhusiwa kutoka Hospitalini ambapo Daktari wa kikosi cha Simba Yassin Gembe amesema atafanyiwa vipimo zaidi kubaini ukubwa wa majeraha aliyopata

"Mkude kwa sasa anaendelea vizuri na ametoka hospitali, isipokuwa anahitaji kufanyiwa vipimo zaidi," Dk Gembe aliiambia tovuti ya klabu ya Simba

Hivi karibuni Mkude alitahadharisha kuhusu uwezekano wa wachezaji kupata majeraha pale ligi itakaporejea baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na ugonjwa wa corona

Tunamtakia kila la kheri aweze kupona haraka na kurejea kwa wakati kuendelea na majukumu yake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’