Mabingwa wa nchi Simba wamewatuliza wababe wa Yanga, KMC baada ya kuwafunga mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju
Pamoja na kucheza mechi nyingine asubuhi ya leo, kikosi cha Simba kimeoneka kuwa tayari kuendeleza mwendo wa dozi kwenye ligi wakionyesha kiwango safi mbele ya watoto hao wa Kinondoni ambao siku ya jana waliwalaza mapema mashabiki wa Yanga kwa ushindi wa mabao 3-0
Nahodha John Bocco ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo baada ya kuweka kambani mabao mawili huku lile la tatu likifungwa na Ibrahim Ajib
Asubuhi Simba ilicheza na Transit Camp na ikafanikiwa kushinda mabao 4-2
Wachezaji wote wa Simba walipata nafasi kwenye michezo hiyo

ADVERTISE HERE