Mkude atahadharisha wingi wa majeruhi ligi ikirejea

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Jun 2020
Mkude atahadharisha wingi wa majeruhi ligi ikirejea

Kiungo mahiri wa Simba Jonas Mkude amesema majeraha yatakuwa mengi kwa wachezaji pale ligi itakaporejea kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu huku wakifanya mazoezi ya aina moja

Ratiba ya Ligi Kuu kurejea, imetolewa mwanzoni mwa wiki Simba ikitarajiwa kuanzia uwanja wa Taifa Juni 14 kwa kuumana na Ruvu Shooting

Mkude amesema wakati wa mapumziko ya corona, wachezaji walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu jambo ambalo huenda litawasumbua pale ligi itakaporejea

Hata hivyo Mkude amesema yeye binafsi anafanya mazoezi kwa kufuata maelekezo anayopewa na makocha wake ili kuhakikisha anajiepusha na changamoto hiyo

"Wakati huu tunapofanya mazoezi ya timu tunahitaji kuwa waangalifu kuepuka majeraha ili kuifanya miili yetu iwe tayari kwa ajili ya mechi zinazokuja mbeleni. Ndio maana hata mwanzoni mwa msimu makocha hutoa program tofauti ya mazoezi ili kujenga, ufit, stamina na mengineyo," alisema

"Kwa wale ambao hawatafanya mazoezi sahihi wakati huu, watakuwa na wakati mgumu ligi ikianza. Kwa upande wetu Simba makocha wetu wako makini, tunafanya mazoezi ambayo yatatusaidia kuwa timamu kimwili tayari kumalizia mechi zilizobaki"

Katika mechi 10 zilizobaki, Simba itahitaji kushinda angalau mechi tano ili kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
10h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
10h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
13h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’