Uongozi wa Simba umerudisha utaratibu wa kuwakata mshahara wachezaji ambao wanapatikana na hatia ya makosa ya utovu wa nidhamu, imefahamika
Uamuzi huo umefikiwa baada ya sakata la hivi karibuni kati ya kocha Sven vandenbroeck na kiungo Ibrahim Ajibu ambaye wiki iliyopita alizuiwa kuingia kambini baada ya kuchelewa
Pamoja na adhabu aliyopewa na Sven, fundi huyo wa mpira amekumbana na adhabu nyingine ya kukatwa sehemu ya mshahara wake
Inaelezwa utaratibu huo umewekewa mkazo Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa ambaye anaamini utawafanya wachezaji wawe makini katika kutimiza majukumu yao
"Ajibu amerejea kikosini lakini atakatwa laki mbili kwenye mshahara wake, ni utaratibu ambao umewekwa kama sehemu ya adhabu kwa wachezaji ambao watakabiliwa na makosa ya kawaida ya kinidhamu," alisema mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba
Kwa wale wanaofuatilia ligi mbalimbali barani Ulaya, utaratibu huu umekuwa ukitumika kwenye ligi hizo