Msemaji na Mkuu wa kitengo cha habari klabu ya Simba Haji Manara amesema baada ya kudumu kwa takribani miaka mitano kwenye nafasi hiyo, utafika wakati ataondoka ili kuwapisha wengine na yeye kusaka changamoto nyingine
Manara anatajwa kuwa Msemaji aliyeipa heshima nafasi hiyo kwani hapo awali Maafisa wa Habari wa vilabu hawakuonekana kuwa na umuhimu mkubwa
Ubunifu na hamasa ambazo anafanya, zimekuwa chachu, kuwa mtu muhimu sana katika klabu ya Simba na haishangazi kuona amekuwa mtu maarufu sana ndani na nje ya nchi
Mwaka juzi kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa wakati Simba ikijaza uwanja wa Taifa katika kila mchezo waliocheza nyumbani, Manara alihusika kwa kiasi kikubwa katika kuhamasisha mashabiki na pengine umaaarufu wake uliongezeka mara dufu baada ya michuano ile
Akiongea jana katika insta Live na Sabrina Golden Hour, alisema kuwa baada ya kudumu na Simba kwa miaka mitano, anawaza kutafuta kazi mpya ya kufanya ili apate changamoto mpya