Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameuagiza uongozi wa mabingwa hao wa nchi kumtafutia angalau mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuanza kwa mikiki mikiki ya ligi kuu
Sven amesema baada ya kufanya mazoezi kwa takribani wiki nzima, anahitaji kuwapima wachezaji wake kabla ya mchezo wa mashindano
"Tunahitaji kupata angalau mchezo mmoja wa kirafiki. Tumezungumza na viongozi, wao ndio watafahamu ni timu gani tutacheza nayo na siku ya mchezo huo kupigwa," alisema Sven baada ya mazoezi jana jioni
Simba inaendelea kujifua katika uwanja wake wa Mo Simba Arena wakijiweka tayari kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo
ADVERTISE HERE