Viungo mafundi wa Simba Francis Kahata na Ibrahim Ajibu leo wamejumuishwa na wachezaji wengine kuendelea na mazoezi ya timu
Ajibu na Kahata walichelewa kuingia kambini kutokana na changamoto zilizowakabili hivyo kocha Sven Vandenbroeck kuwaandalia mazoezi ya peke yao
Nyota hao wamemaliza program hizo na Sven kawarudisha kwenye timu ya kwanza
Mabingwa hao wa nchi wameendelea na mazoezi katika uwanja wao wa Mo Simba Arena kujiweka sawa tayari kutetea ubingwa wao kwa msimu wa tatu mfululizo


ADVERTISE HERE